By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: Tunawaondoa watoto kwenye ajira na kuwarejesha shuleni-CAMFED
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Uncategorized > Tunawaondoa watoto kwenye ajira na kuwarejesha shuleni-CAMFED
Uncategorized

Tunawaondoa watoto kwenye ajira na kuwarejesha shuleni-CAMFED

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:31 PM
By Tanzania Kids Time 2 Min Read
Share
SHARE

 

Shirika lisilo la kiserikali la CAMFED nchini Tanzania linaendeleza harakati za kutetea haki za watoto, hususani wa kike, kuwaondoa kwenye ajira za utotoni na kusaidia kuwarejesha shuleni.  

Zamoyoni Selemani ni Mratibu wa Miradi wa CAMFED halmashauri ya wilaya ya Kilosa na Gairo, “miradi yetu imejikita sana katika kumsaidia mtoto wa kike, katika elimu yake lakini hatuishii katika elimu. Vilevile kwa mto wa kike ambaye ameshamaliza shule, tunamwendeleza katika vyuo vya ufundi, lakini pia tunawapeleka katika vyuo vya kati, ngazi ya cheti na diploma, lakini pia wale ambao hawana sifa za kwenda vyuo tunawapa miradi ambayo wanaweza wakafanya biashara zao katika kata zao, hii yote ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike hawezi kuwa tegemezi katika mazingira ya sasa.” 

Asha ni mnufaika wa mradi huu na sasa amekuwa muelimishaji anayewasaidia wengine kama yeye ambao kutokana na sababu mbalimbali wamejikuta wakiishi katika mazingira magumu. Asha anasema, “mimi kama msichana nimepitia huko kwa sababu baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari, baba alikuwa na matatizo yaliyompelekea kuugua kwa muda mrefu. Kwa hivyo ikanibidi niende kutafuta kazi, nikaajiriwa.”  

Mwalimu Elisifa Nasali ni mwalimu katika sekondari ya Kimamba na pia ndiye mlezi wa wanafunzi wanufaika wa mradi wa CAMFED anasema, wengi kama Asha wamenufaika lakini uhitaji bado ni mkubwa, “watoto ni wengi ambao wana shida. Wengi sana ambao wana shida na wana uhitaji. Ingewezekana tungeongezewa hata namba ya watoto ambao wangepata msaada.” 

Tumaini Geugeu ni Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Kilosa, anaeleza namna wanavoshirikiana na mashirika kama haya yasiyo ya kiserikali, pamoja na jamii, “sisi kama serikali, kitu kikubwa ambacho tunakifanya, cha kwanza ni kuzunguka kwenye maeneo au mitaakutoa elimu kwa wazazi, vijana na jamii kwa ujumla. Inasaidia, mtu wa kawaida anapomwona mtoto ambaye amebeba biashara wakati wa mda wa shule kututafuta na kutupa taarifa moja kwa moja.”

Komesha utumikishwaji wa watoto kwenye jamii yako,ilikuleta usawa katika jamii.


Na.John Kabambala. 

You Might Also Like

ENERGY AND NEO-COLONIALISM IN AFRICA, NO ANSWERS?

WAHITIMU WATAKAO JIUNGA DARASA LA KWANZA MWAKA 2023

ATHARI ZA NDOA ZA UTOTONI KIUCHUMI

SIKU YA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA KUKOMAA

ATHARI ZA NDOA ZA UTOTONI KIELIMU

Tanzania Kids Time December 7, 2020
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article Dhamira ya kwanza ya kipekee kabisa ya kuondoa saratani ya shingo ya kizazi
Next Article IDADI YA WATOTO TANZANIA MWAKA 2014.
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?