Pichani ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Morogoro Paul Joel Ngwembe akiwa Meza kuu.
Mahakama kuu kanda mpya ya Morogoro imeweka mikakati ya
kumlinda mtoto, kwa kutoa Elimu ya ulinzi wa mtoto kwa wananchi ili kupunguza
matukio ya ukatili dhidi yao.
Dhamira hiyo ilielezwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu
kanda ya Morogoro Mheshimiwa PAULO
NGWEMBE, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini iliyofanyika Uwanja wa
Jamhuri Mkoa wa Morogoro.
Mheshimiwa PAULO NGWEMBE ambaye anatoka kituo cha Haki
jumishi kanda ya Morogoro, amesema matukio ya ukatili kwa watoto yamekithili
ndio maana wamewekeza nguvu kutoa Elimu kwa wananchi ili kumlinda mtoto.
‘’Mmeona matukio
mengi siku hizi yanatokea matukio mengi yanatokea, watoto wamebakwa, watoto
wameuwawa, sasa tunatoa Elimu ya Sheria kwa namna hiyo ili jamii iwe na
uelewa’’ alisema PAULO NGWEMBE.
Nae Naibu msajili wa Mahakama kuu Kanda ya Morogoro
SYLVESTER KAINDA alisema ‘’watoto ambao
ni Taifa la kesho ni lazima walindwe sio tu na Sheria bali hata kijamii,
tusiachie tu Sheria kwa sababu mmomonyoko wa maadili pia unapelekea uwepo wa
matukio hatari sana kwa watoto hasa wa kike, tushirikiane kwa pamoja kupinga
vitendo hatari kwa maendeleo ya Mtoto’’.
Hafla ya uzinduzi wa wiki ya Sheria ilihusisha Bonanza la
michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, Draft, Bao, Kuvuta Kamba, Kukimbia na Gunia,
Kukimbiza Kuku, mchezo wa Karata na Mpira wa miguu.
Wiki ya Sheria Nchini ilizinduliwa kitaifa Makao makuu ya Mahakama
Tanzania, Jijini Dodoma na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar HUSSEIN ALLY MWINYI na inatarajia kuhitimishwa Tarehe Mosi mwezi wa Pili 2022, ikiongozwa na
kaulimbiu isemayo ‘’zama za mapinduzi ya nne ya viwanda, safari ya maboresho kuelekea
mahakama mtandaoni’’.
Na Hamad Rashid – Morogoro.