Jamii imekumbushwa kuona umuhimu wa kuwajali wanawake
wajane ambao mara kadhaa wamekua wakikosa msaada katika familia zao baada ya
kufiwa na waume wao ili na wao waishi maisha ya furaha sawa na wengine.
Mwishoni mwa Mwaka 2021 Mwezi Disemba Tanzania kids
time ilihudhuria Mkutano wa wanawake wajane 130, waliopewa mafunzo Mkoani
Morogoro wakifundishwa jinsi ya kuishi maisha baada ya kufiwa na waume wao.
Ikiwa ni Mwaka wa Tisa tukio hili linafanyika, ambapo
Mwaka 2021 lilifanyika ndani ya Ukumbi wa wa Mikutano wa La Miriam uliyopo
Mjini Morogoro, wajane 130 wamehudhuria mafunzo ya siku Saba wakipewa Elimu ya
nama ya kuishi maisha baada ya kufiwa ikiwemo kujitahidi kujali Afya zao,
matumizi ya vyakuala asilia, kuwa na upendo pamoja na kujishughulisha na kazi
mbalimbali za kujipatia kipato.
Mafundisho waliyopata wajane yaliwapa faraja na kujiona
kuwa ni Jasiri na sio wanyonge tena, walisimulia Amina Mbwana Mjane kutoka
Kisalawe, Pwani na Edith Chitukuro Mjane kutoka Jiji la Dodoma ,walipohojiwa na
Tanzania Kids Time.
Amina
Mbwana alisema “tumekutanishwa hapa kututoa ule msongo
wa mawazo kwamba kufika ni balaa lakini kumbe kufiwa ni jambo la kawaida, watu
walikua wanakaa wakilia, kumbe hutakiwi kulia inabidi umwamini Mungu na kusonga
mbele”
Mkutano huu umeweza kututia faraja kwa yale mafunzo
ambayo tumeweza kupewa, tumeambiwa wajane sio watu wa kulia, ndio jambo ambalo
nimejifunza” alisema Edith Chitukuro
Mjane kutoka Mkoa wa Dodoma.
Miongoni mwa wawezeshaji wa Mafunzo katika Semina hiyo
ya wajane ni Mjane na mwanasheria mstaafu Ester Mtaki kutoka Mkoa wa Mwanza na
Tabibu wa magonjwa ya Binadamu David Lugomela Mkazi wa Morogoro, kwa pamoja
walijikita kuwafundisha wajane kujali Afya ya Macho pamoja na kutokalia haki
zao badala yake wawe wakifuata Sheria kupata Haki zao.
Mhutubu mkuu wa Mkutano Simbarashe Charumbira kutoka
nchini Canada nae alieleza changamoto zinazowasumbua wanawake wajane ikiwemo
kukosa kushughulisha akili wakiamini wao ni watu wa kusaidiwa kila siku.
“Tumekua hapa kwa ajili ya mkutano huu wa wajane
tumejifunza mengi na nitumie fursa hii kuwahamasiha wajane wengine walioko
Nyumbani wakati mwingine waweze kushiriki, nilichokiona kwa wajane hawapendi
kutumia akili zao lakini pia tumewafundisha vitu vya kufanya Nyumbani kwao ili
kuimarisha Afya zao ili waishi maisha mazuri” alisema Simbarashe Charumbira
Neema Tuvako ndiye mratibu wa Semina hii iliyopewa
jina la Muendelezo wa maisha ya wajane.
“lengo langu kabisa ifike mahali Jamii ione umuhimu wa
kujali wajane wao, kwasababu kwakweli anayemtesa Mjane sio Mtu wa mbali, ni Mtu
wa Jamii, ni Mtu wa Familia kwa hiyo Jamii ifike mahali ithamini wajane wao,
ithamini wale watoto, sisi tunaamini kwamba ukimsaidia mjane mmoja naye anaweza
kusaidia Yatima wake” alisema Neema
Tuvako.